Our Team

OUR TEAM

Ugugaji Bora Group ina timu ya wataalamu waliobobea katika sekta ya ufugaji, wakiwemo:

  • Mafunzo: Wataalamu wa kutoa mafunzo na elimu ya kina kwa wafugaji.
  • Mifugo: Wataalamu wa kushauri kuchagua na kupata mifugo bora na yenye afya.
  • Vifaa: Wataalamu wa kushauri upatikanaji wa vifaa bora vya ufugaji.
  • Ushauri wa Kidigitali katika ufugaji na masoko: Wataalamu wa kutoa ushauri wa kidigitali na msaada kwa wafugaji.

Ugugaji Bora Group ina timu yenye uzoefu na utaalam katika nyanja mbalimbali za ufugaji. Timu yetu inajumuisha wataalam wa ufugaji wa wanyama na ndege, wataalamu wa lishe ya mifugo, madaktari wa mifugo, na wataalamu wa kilimo cha kisasa. Kila mjumbe wa timu yetu amepewa mafunzo ya kina na ana uzoefu wa miaka mingi katika sekta ya ufugaji(Naye pia ni mfugaji).

OUR COMMITMENT

Tunajitolea kwa dhati kuhakikisha wafugaji wanapata huduma bora na ya kipekee ambayo itawasaidia kuboresha mbinu zao za ufugaji na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku. Kwa ushirikiano na wafugaji na wadau mbalimbali, tunaamini tunaweza kubadilisha na kuboresha sekta ya ufugaji kwa manufaa ya wote.

UFUGAJIBORA GROUP

Ugugaji Bora Group tunajitahidi kuwa mshirika wako wa kweli katika safari yako ya kufikia mafanikio katika ufugaji. Tunaamini katika nguvu ya ushirikiano na uaminifu katika kuboresha maisha ya wafugaji na jamii nzima.