About Us Basic

KUHUSU UFUGAJI BORA GROUP

Ugugaji Bora Group ni kikundi cha wataalamu wa ufugaji, wajasiriamali, na wafugaji wenye malengo ya pamoja ya kuboresha sekta ya ufugaji nchini Tanzania na kwingineko. Tunajivunia kuwa na timu yenye uzoefu mkubwa katika nyanja mbalimbali za ufugaji, ikijumuisha mafunzo, ushauri wa kidigitali, na ushauri wa upatikanaji wa mifugo na vifaa bora vya ufugaji.

Ugugaji Bora Group ilianza mwaka 2014 kwa lengo la kujenga jamii yenye wafugaji bora na wenye ufanisi.

Ugugaji Bora Group ilisajiliwa rasmi mwezi Machi 2021 na imesajiliwa na Brella chini ya namba ya usajili 48937.

OUR MISSION

Kutoa elimu ya kina na mafunzo kwa wafugaji ili waweze kuboresha mbinu zao za ufugaji, kusaidia kupata mifugo yenye ubora wa hali ya juu, na kuwezesha upatikanaji wa vifaa bora vya ufugaji ili kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa za mifugo.

OUR VISION

Kuwa kiongozi wa kimataifa katika kutoa mafunzo bora ya ufugaji, kuwasaidia wafugaji kupata mifugo bora, na kushauri wafugaji upatikanaji wa vifaa bora vya ufugaji kwa ajili ya kuboresha maisha na kupata faida.

OUR SUCCESS RATE

WHAT WE HAVE DONE

Katika Ufugaji Bora Group, tunajivunia kiwango cha juu cha mafanikio katika kutoa elimu na kusaidia wafugaji kuboresha uzalishaji wao na kuleta maendeleo endelevu.

20+

Elimu ya ufugaji wa mifugo mingi

100+

Kusaidia kuagiza vifaa na zana

4.9+

AVERAGE RATINGS

50+

Mifugo iliyo bora