Tunatoa Elimu Kupitia Mitandao na Website pia elimu ya vitendo kwa kutembelea mashamba yetu Salasala na Mabwepande: Tunatoa elimu  inazolenga kuboresha ujuzi wa wafugaji katika nyanja tofauti za ufugaji.

Tunatoa elimu kwa ufugaji wa wanyama mbalimbali:

  • Ufugaji Bora wa Ng’ombe: Kujifunza mbinu bora za kutunza na kuzalisha ng’ombe wenye afya na wenye tija.
  • Ufugaji Bora wa Mbuzi: Kupata maarifa juu ya mbinu bora za ufugaji wa mbuzi kwa ajili ya nyama, maziwa, na ngozi.
  • Ufugaji Bora wa Kondoo: Kujifunza jinsi ya kufuga kondoo kwa ajili ya kuzalisha manyoya, nyama, na bidhaa nyingine.
  • Ufugaji Bora wa Kuku: Kupata ujuzi juu ya mbinu bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji na wa kisasa kwa ajili ya mayai na nyama.
  • Ufugaji Bora wa Samaki: Kujifunza mbinu bora za ufugaji wa samaki kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kipato.
  • Ufugaji Bora wa Simbilisi (Guinea Pigs): Kupata maarifa juu ya mbinu bora za kufuga simbilisi kwa ajili ya biashara na kama wanyama wa kipenzi.
  • Ufugaji Bora wa Sungura: Kujifunza mbinu bora za ufugaji wa sungura kwa ajili ya nyama na manyoya.
  • Ufugaji Bora wa Kanga: Kupata ujuzi wa jinsi ya kufuga kanga kwa ajili ya nyama, mayai, na kama wanyama wa mapambo.
  • Ufugaji Bora wa Bata: Kujifunza mbinu bora za ufugaji wa bata wa kienyeji, Muscovy, na Pekin kwa ajili ya nyama, mayai, na manyoya.

Mafunzo ya Vitendo

Tunatoa mafunzo ya vitendo katika mashamba yetu ya mfano ili wafugaji waweze kujifunza kwa kuona na kufanya wenyewe. Katika mafunzo haya, wafugaji watapata fursa ya:

  • Kujifunza Kwa Vitendo: Kupata uzoefu wa moja kwa moja kwa kushiriki katika shughuli za kila siku za ufugaji.
  • Kushiriki Katika Kazi za Kila Siku: Kuona na kujifunza jinsi ya kutekeleza kazi mbalimbali za ufugaji kama vile kulisha, kutibu wanyama, na kudhibiti magonjwa.
  • Mafunzo ya Kitaalamu: Kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa mifugo juu ya mbinu bora za ufugaji na usimamizi wa mifugo.

Kwa njia hizi, tunalenga kuwajengea wafugaji ujuzi na maarifa ya kisasa ili waweze kuboresha uzalishaji na kipato katika shughuli zao za ufugaji bora.

Service brochure

Kwa njia hizi, tunalenga kuhakikisha kuwa mifugo yako inakuwa na afya bora, kuongeza uzalishaji, na kuboresha kipato chako.

Mafunzo na ushauri wa afya ya mifugo

Tunatoa ushauri kuhusu jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa mbalimbali ya mifugo, pamoja na kutoa chanjo muhimu kwa mifugo.

  • Utunzaji Bora wa Afya ya Mifugo
  • SChanjo na Matibabu
  • Udhibiti wa Magonjwa
  • Ushauri wa Lishe
  • Mazoezi na Mazingira Bora
  • Usimamizi wa Uzazi
  • Usafi na Utunzaji wa Mazingira
  • Matumizi ya Dawa na Viua Vijasumu

Tunatoa Elimu Kupitia Website Yetu, Mitandao ya Kijamii, na Magroup ya Ufugaji:

Katika Ugugaji Bora Group, tuna uzoefu wa kutosha kusaidia wafugaji kukabiliana na changamoto mbalimbali. Timu yetu ya wataalam imejitolea kujibu maswali yote ya wafugaji na kutoa msaada wa haraka na wa kina ili kuhakikisha mafanikio ya shughuli zao za ufugaji.