Tunasaidia Wafugaji Kutafuta Masoko ya Mifugo Yao:

Tunatoa msaada kwa wafugaji ili kuhakikisha kwamba mifugo yao na bidhaa zinazotokana nayo, kama vile nyama, maziwa, na mayai, zinafikia masoko bora. Tunawasaidia kufanya utafiti wa soko ili kubaini mahitaji ya wateja na kuunganisha na wateja wa jumla na rejareja ambao wanahitaji bidhaa zao.

Kuunganisha wafugaji

Kuwaunganisha Wafugaji katika Magroup:

Tunawaunganisha wafugaji katika magroup maalum kwa aina ya mifugo wanayofuga na maeneo yao. Magroup haya yanawaruhusu wafugaji kubadilishana mawazo, kushirikiana katika kutatua changamoto, na kupata ushauri kutoka kwa wenzao.

Kuwaunganisha Wafugaji Kufahamiana:

Tunaratibu mikutano na warsha ambapo wafugaji wanaweza kukutana na kufahamiana. Hii inawasaidia kujenga mitandao ya kijamii na kibiashara, ambayo ni muhimu kwa kuboresha shughuli zao za ufugaji na kuongeza fursa za soko.

Service brochure

Kwa msaada huu, wafugaji wataweza kupanua masoko yao, kuboresha mitandao yao, na kutumia teknolojia ya kisasa kujitangaza na kuuza bidhaa zao kwa ufanisi zaidi.

Kusaidia Wafugaji Kujitangaza katika Social Media:

Tunawasaidia wafugaji kujitangaza kupitia majukwaa ya kijamii kama Facebook, Instagram, na WhatsApp. Tunatoa mafunzo juu ya jinsi ya kuunda na kusimamia akaunti za biashara, kuweka matangazo, na kushirikisha wateja. Hii inawawezesha wafugaji kufikia wateja wengi zaidi na kuongeza mauzo yao.

  • Kusaidia na kuwafundisha wafugaji kujitangaza katika mitandao ya kijamii
  • Kujitangaza katika magroup
  • Kufikia wateja wapya katika mitandao
  • Kuboresha mauzo
  • Kufundisha wafugaji mikakati ya kuchunguza fursa za soko
  • Kuendelea kuwatafiutia wafugaji masoko ya nje ya nchi